Thursday, October 27, 2016

DC ATOA SIKU 10 KWA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI BOMBA MATALA

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na wananchi wa kijiji cha Matala 











Diwani wa kata ya Mtenga Mh. Pankras Maliyatabu akiongea na wananchi wa kijiji cha Matala
Afisa mtendaji wa kata ya Mtenga Bwana Joshua Mwimanzi akiwahimiza wananchi wa kijiji cha Matala kujikita zaidi katika shughuli za maendeleo

Afisa tarafa ya Namanyere Bwana Kassim Abdul akitambulisha viongozi wa serikali walioambatana na mkuu wa wilaya katika ziara 
Afisa mtendaji wa kijiji cha Matala Bwana Revocatus Tinga akijibu maswali yaliyo ulizwa na mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda
Mhandisi wa maji Bwana Francis Mapunda akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa maji kijiji cha Matala
Mkandarasi wa mradi wa maji kijiji cha Matala Bwana Jofrey Godfrey akifanya mawasiliano na mmoja wa wahusika katika ujenzi wa mradi

 Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akiongea na wananchi wa kijiji cha Matala katika mkutano wa hadhara

Bwana Silvanus Malisela mkazi wa kijiji cha Matala akiuliza swali juu ya ubovu wa miundo mbinu ya barabara inayotoka kijiji cha Mtenga mpaka katika kijiji cha Matala
Bwana Claudio Kastiko mkazi wa kijiji cha Matala akiomba ufafanuzi kuhusu wafugaji wafugaji wanao kaidi agizo la serikali


 Bi Lishada Melimeli mkazi wa kijiji cha Matala akihoji juu ya fedha za mikopo ya vikundi vya akina mama zilizo takiwa kutolewa kwa mujibu wa ahadi ya Mh. Rais Magufuli




Bonyeza ili kutazama video ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akiwahoji Mhandisi wa maji na Mkandarasi wa mradi katika mkutano wa hadhara


Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda ametoa siku 10 kwa mkandarasi wa mradi wa maji bomba Bwana Jofrey Godfrey na Mhandisi wa maji Bwana Francis Mapunda kukamilisha mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Matala wilayani Nkasi mkoani Rukwa
Akiongea alhamisi hii katika mkutano wa hadhara mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda amesema mradi huo umekuwa ukisuasua muda mrefu bila mafanikio na kuwataka kuukamilisha mradi huo ndani ya mwezi mmoja na kuahidi kutembelea mradi huo baada ya siku 10 ambapo mkandarasi wa mradi huo amedai kutumia siku 7 kukamilisha mfumo wa umeme jua kwa ajili ya uendeshaji wa mashine ya kuvuta maji
Amesema pamoja na kuwepo fedha kwenye akaunti kwa ajili ya mradi huo bado utekelezaji wa mradi huo umekuwa ukitekelezwa chini ya kiwango na mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi milioni 422 na mpaka sasa mkandarasi tayari ameshalipwa shilingi milioni 258
Akiwa katika ziara ya ukaguzi wa mradi wa maji mkuu huyo wa wilaya ya Nkasi Mh. Mtanda ametumia ziara hiyo kutoa Jenereta katika shule ya msingi Matala ili kuwapa wanafunzi uwezo wa kujisomea wakati wa usiku


No comments:

Post a Comment