Thursday, September 29, 2016

DC AHUDHURIA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI KAZOVU




Bonyeza ili kutazama video ya Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda akiwa katika mahafali ya kidato cha nne Shule ya sekondari Kazovu
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda (katikati) akitembelea mazingira ya Shule ya sekondari Kazovu


Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda (katikati) na kulia ni Kaimu Afisa tawala wa wilaya Bwana Kassim Abdul (kushoto) ni Mkuu wa Shule ya sekondari Kazovu Bwana  Elieza Dononda

Mkuu wa shule ya sekondari Kazovu Bwana Elieza Dononda akisoma ratiba ya mahafali ya kidato cha nne

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Kazovu pamoja na wageni waalikwa katika mahafali ya kidato cha nne
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda akipiga picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Kazovu na wanafunzi wa kidato cha nne
Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kazovu
Mkuu wa shule ya sekondari Kazovu na Makamu wa shule wakisoma taarifa ya shule

Wanafunzi wa kidato cha nne wakisoma taarifa ya Wanafunzi wa shule ya sekondari Kazovu

Kwaya ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kazovu


Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda akigawa vyeti kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika mahafali yaliyofanyika katika shule ya sekondari Kazovu
Wageni waalikwa wakiwa katika mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari Kazovu
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda amewataka walimu wa shule ya sekonadari Kazovu iliopo kijiji cha Kazovu Wilayani Nkasi mkoani Rukwa kuwapa kipaumbele kimasomo wanafunzi wa kike ili waweze kuwa viongozi wa baadae.
Ameyasema hayo mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanada jumatano ya wiki hii katika mahafali ya kidato cha nne yaliyofanyika katika shule ya sekondari Kazovu ambapo amezungumzia changamoto zinazo wakabili watoto wa kike ni pamoja na kutopewa kipaumbele katika masomo mashuleni
Aidha mkuu huyo wa wilaya aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne ambayo ni mahafali ya pili kwa shule hiyo tangu ilipofunguliwa mwaka 2009 kupitia arambee iliyofanyika katika mahafali hayo aliweza kuchangia kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya maendeleo ya shule hiyo
Kupitia mahafali hayo mkuu huyo wa wilaya Mh Mtanda amekemea kuwapo kwa mahusiano yanayo wahusisha Walimu na wanafunzi katika shule hiyo na kwamba atafanya uchunguzi ili kuweza kuwabaini Walimu wenye tabia hiyo na kuwachukulia hatua za kinidhamu pia kuwachukulia hatua wazazi wanao waoza wanafunzi kabla ya kumaliza masomo
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Bwana Elieza Dononda amewataka wananchi wa kijiji cha Kazovu kutoa ushirikiano katika maendeleo ya shule hiyo ambapo wazazi wa kata hiyo wanashiriki katika ujenzi wa shule kwa asilimia 20% kati ya asilimia 100%  na wanafunzi wa shule hiyo wanaotokea kwenye kata hiyo wanapunguzo la ada
Katika taarifa ya shule hiyo iliyosomwa na mkuu wa shule Bwana Elieza na makamu wake Pascharia Joseph wamesema mnamo mwaka 2015 shule imeweza kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya kidato cha nne kimkoa




No comments:

Post a Comment