Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh Said Mohamed Mtanda (kulia) akiwa na maofisa ardhi ofisini kwake (wa kwanza kushoto) mkuu wa idara ya ardhi Emmanuel Kushoka |
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda (katikati) akitoa agizo kwa ofisa ardhi wakati wakielekea katika eneo la viwanja |
Wananchi wa eneo la Majengo A wakiongea na mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh Said Mtanda
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akiongea na wananchi wa eneo la Majengo A
|
Baadhi ya wananchi wa eneo la Majengo A wakiwa ofisini kwa mkuu wa wilaya |
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda ameanza leo kusimamia zoezi la ugawaji wa viwanja lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na wananchi wa kata ya Majengo A wilayani Nkasi mkoani Rukwa baada ya kuiagiza idara ya ardhi kitengo cha upimaji viwanja kuhakikisha viwanja vinapimwa kwa wakati na wahusika kupewa viwanja vyao.
Eneo hilo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu toka serikali itoe tangazo la kupima mashamba hayo lakini zoezi hilo llilmekuwa gumu kutekelezeka kiasi cha wananchi wa eneo hilo kuomba msaada kwa mkuu wa wilaya Mh. Said Mtand
Akiwa katika eneo hilo mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda na wataalam kutoka idara ya ardhi kitengo cha upimaji viwanja amewataka wananchi hao kuhakikisha wana yaendeleza maeneo yao ya viwanja kwa muda usiopungua miezi 36 na atakaye kaidi agizo hilo eneo lake litachukuliwa na serikali.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia muda huo pia kutoa onyo kwa baadhi ya watendaji wa idara ya ardhi wanaofanya kazi kwa mazoea na kuwataka kuwa na uadilifu katika kutimiza majukumu yao ya kazi ili kuepusha migogoro inayotokana na kutokuwa makini
Mmoja wa wananchi hao ambaye amekuwa akisubiri kukamilika kwa zoezi hilo kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote amemshukuru na kumpongeza mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh.Mtanda kwa juhudi kubwa alizofanya mpaka kuhakikisha wananchi hao wanapewa viwanja vyao.
No comments:
Post a Comment