Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akisisitiza juu ya ukusanyaji wa mapato ya ndani |
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiwasikiliza watendaji wa kata kwa umakini |
Watendaji wa kata wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda katika ukumbi wa Halmashauri wilayani Nkasi |
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi Julius Mseleche Kaondo akitoa ufafanuzi juu ya ukusanyaji mapato ya ndani kwa watendaji wa kata |
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mh. Zeno Sumuni Mwanakulya |
Afisa mtendaji wa kata ya Majengo wilayani Nkasi Rock Msalange akizungumzia juu ya changamoto zilizopo katika ukusanyaji mapato |
MKUU wa
wilaya Nkasi Said Mohammed Mtanda amesema kuwa uwezekano wa halmashauri ya
wilaya Nkasi kuvuka malengo yake ya ukusanyajli wa mapato inawezekana klamla
watendaji watabadilika na kuafanya kazi kwa mazingira ya uadillifu
Akizungumza
na maafisa watendaji wa kata kwenye kikao chao cha kazi mkuu huyo wa wilaya
amesema kuwa amefanya ziara za kushitukiza katika maeneo mbalimbali ya ukusanyaji
wa mapato na kubaini mianya mingi inayoikosesha mapato halmashauri na kuwa sasa
ni wakati wa kujituma kufanya kazi na atakayezembea kama uzembe unaoonekana sasa miongoni mwa
watendaji hawatavumiliana bali hatua stahiki zitachukuliwa.
Amesema moja
ya dhambi kubwa kwa mtendaji wa serikali ni pale mtendaji anapovunja sheria na
kupelekea kupotea kwa mapato ya
hamashauri na kuwa mtendaji wa namna hiyo ni lazima achukuliwe hatua stahiki za
kinidhamu.
Mkuu huyo wa
wilaya ametaka wakuu wa idara mbalimbali
za halmashauri kufanya ziara za kushitukiza katika maeneo mbalimbali ya wilaya
na kufanya ukaguzi kwa watumishi walio
chini yao na kuwa kwa kufanya hivyo watabaini mambo kadha wa kadha na kuweza
kuyafanyia kazi baadhi ya mambo wanayoyakuta pale kama hayaendi vizuri na
kuchukua hatua za haraka pale pale
Na kudai
kuwa ameagiza watendaji wa kata na vijiji
kuhakikisha kuwa wanawakamata wahamiaji haramu waliovamia katika nchi
hii hususani mwambao mwa ziwa Tanganyika ili kuleta utengamavu na utulivu
katika nchi hii.
Mkurugenzi
mtendaji Julius Mseleche Kaondo kwa upande wake amesema kuwa kikao hicho
kimelenga kukumbushana mambo mengi ya msingi na kuwa mengi aliyoyasema mkuu wa
wilaya ndiyo wamekua wakikumbusha na kila wakati na kuwa kila jambo ni muhimu
kulifanyia kazi
No comments:
Post a Comment