BWENI la Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nkomolo wilayani Nkasi mkoani Rukwa
limeteketea kwa moto huku wanafunzi wakinusurika.
Moto huo umetokea jana majira ya saa mbili usiku wakati
wanafunzi hao walipokuwa darasani wakijisomea huku bweni na vifaa vilivyomo
vyote kuteketea kwa moto
Akizungumza jana mkuu wa wilaya ya Nkasi Said Mohammed Mtanda alisema kuwa baada ya
moto huo kuwaka katika bweni hilo wananchi walijitokeza kwa wingi kuanza
kuuzima moto huo ingawa juhudi hizo hazikuzaa matunda .
Alisema kuwa uwezo wa
bweni hilo ni kuchukua wanafunzi 48
lakini wanafunzi waliokuwa wakilitumia bweni walikua ni 14 ambapo wengine
walihamishiwa mabweni mengine kabla ya moto huo kutokea.
Mkuu huyo wa wilaya alidai kuwa serikali baada ya uchunguzi wake imebaini
kuwa moto huo umetokea baada ya Chemry moja ndani ya bweni hilo kupasuka.
Alidai kuwa kimsingi moto huo umetokea kwa sababu za uzembe
kwa waalimu wa shule hiyo kwa kutumia taa ambapo serikali imekataza matumizi ya
taa na mishumaa kwenye mabweni ya Wanafunzi
na pia shule hiyo imebainika kuwa haina Matron kwa muda mrefu
Alisema kwa sasa
wanafunzi hao wanahifadhiwa kwa muda kwenye nyumba ya Matron hadi hapo bweni
hilo litakapojengwa upya
Na ametoa agizo kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya na afisa
elimu kuandika waraka kuziandikia shule zote 14 za bweni kupinga matumizi ya mishumaa ,Taa na pasi za
umeme kwenye mabweni
Mkuu huyo wa wilaya amefafanua kuwa jengo lililoungua lina
thamani ya Tsh,Mil 40 na kuwa sasa wanaangalia ni kiasi gani cha fedha
kinatakiwa kwa sasa kwa ajiri ya ukarabati na kuwa ni jukumu la Wananchi
kuchangia ili bweni hilo liweze kurejea katika hari yake ya kawaida.
Mwisho
No comments:
Post a Comment