Mkuu wa wilaya Mh. Said Mohammed Mtanda akimsikiliza muwezeshaji |
Mbunge wa Nkasi kusini Mh. Desderius Mipata ,Mkurugenzi wa Halmashauri Julius Mseleche Kaondo na Katibu tawala Festo Chonya wakisikiliza maelekezo kutoka kwa muwezeshaji |
Mkurugenzi wa Halmashauri Julius Mseleche Kaondo |
Mkurugenzi wa Halmashauri (kushoto) akiwa naMr. Lucas Mkurugenzi mtendaji kampuni ya JOHN DEERE |
Na Israel Mwaisaka
NKASI
MKUU wa wilaya Nkasi mkoani Rukwa Said mohammed Mtanda akiambatana na viongozi wenzie wa wilaya,Mkurugenzi mtendaji Julius Mseleche Kaondo ,mbunge wa jimbo la Nkasi kusini Desderius mipata Afisa kilim,o wa wilaya Permin Matumizi na Wakopeshaji wa Matrekta ya John Deere wakiwa kwenye shamba la mwekezaji la MSIPAZI FARM
siku hiyo ilikua ni siku ya maonyesho ya zana za kilimo za JOHN DEERE kwa wakulima ambao wamekopa zana za kilimo kupitia shirika hilo la JOHN DEERE
mkuu huyo wa wilaya amewataka Wakulima kubadili mwelekeo wa kilimo na kushiriki kwenye kilimo cha kisasa kinachotumia vifaa vya kisasa.
na aliwataka wakulima kutoogopa kukopa ili waweze kuingia kwenye kilimo chenye ushindani na chenye kuleta tija
shamba hilo la mwekezaji la Msipazi Farm linalomilikiwa na Sumry ni shamba kubwa la uwekezaji ambalo kampuni ya JOHN DEERE imekuwa ikitumia zana zake za kilimo katika shamba hilo na kuitumia siku hiyo kufanya maonyesho ya zana hizo za kilimo kwa wakopaji wa vifaa hivyo chini ya Uangalizi wa Managing director wa JOHN DEERE Mr.Lucas akitoa maelekezo namna ya kutumia vifaa hivyo
PICHA
Picha zote zinaelekeza shughuli zilizofanyika kwenye maonesho ya zana hizo za kilimo chini ya kampuni ya JOHN DEERE
No comments:
Post a Comment