MKUU WA WILAYA AFUNGUA MAFUNZO YA MGAMBO KATA YA MKWAMBA
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda (kushoto) na (kulia) Mshauri wa mgambo wilaya ya Nkasi
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda (katikati)
Wanafunzi wa mafunzo ya mgambo kata ya Mkwamba
Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo ya mgambo akitoa amri kwa wanafunzi wa mafunzo ya mgambo
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akipokea taarifa kutoka kwa mmoja wa wakufunzi wa mgambo
Bonyeza ili kutazama video ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akijitambulisha kwa wananchi wa kijiji cha Swahila na kufungua mafunzo ya mgambo
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akiongea na wanafunzi wa mafunzo ya mgambo
Katibu tawala wa wilaya Bwana Festo Chonya
Mwenyekiti wa kijiji cha Swahila
WAKAZI wa kata ya Mkwamba wilayani nkasi mkoani rukwa wameiomba
serikali kuwapelekea huduma ya kituo cha afya na polisi katika kata hiyo
kutokana na changamoto kadhaa zinazowakabili.
Ombi hilo limetolewa na diwani wa kata hiyo ya Mkwamba
Chiluba Mwandamo kwa mkuu wa wilaya Nkasi Said Mtanda kwenye mikutano tofauti
aliyoifanya jana katika kata hiyo ya Mkwamba.
Amesema kata hiyo jiografia yake ni ngumu kiasi cha wananchi
wa eneo hilo kushindwa kupata huduma za haraka za kiafya baada ya kutokuwepo kituo
cha afya na kuazimikla kuifuata huduma hiyo mbali na wengine ulazimika kufariki
dunia kwa sababu ya kuchellewa kupata huduma hizo za kiafya kwa kwenda umbali
mrefu kufuata kituo cha afya kilipo.
Amesema kutokana na uhitaji wa huduma hiyo ya afya wananchi
wa kijiji cha tambaruka wamefyatua tofali 250,000 kama hakiba na kudai kuwa wao
wapo tayari kuanza kujenga kituo cha afya pale serikali itakaporidhia
Katika hatua nyingine diwani huyo aliomba katika kata hiyo
kijengwe kituo cha poisi hasa baaba ya eneo hilo kuwa na matukio mengi ya
kihalifu na kuwa suluhisho ni kuwa na kituo kidogo cha polisi katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya said Mtanda kwa upande wake amesema serikali
imekisikia kilio hicho na kuwa itakwenda kulifanyia kazi ombi hilo,huku
akipongeza jitihada za wananchi wa kijiji cha Tambaruka ambao wameanza
kufayatua matofali na kuwataka wananchi wengine katika vijiji vyao kuwa na
banki ya matofali ili kuweza kukabiliana na shughuli yoyote ya maendeleo
inayoitajika katika vyao
No comments:
Post a Comment