DC NKASI AAGIZA POLISI KUMKAMATA ALIYE HUSIKA NA MAUWAJI YA MFUGAJI
Bonyeza kuitazama video ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akitoa pole kwa familia ya marehemu pamoja na kutoa agizo kwa polisi
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na Tongejiwe Kuzenza ambaye ni baba mzazi wa marehemu
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akizungumzia taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kuepuka migogoro ya ardhi
Wananchi wa kijiji cha Lyele wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda
Mzee Kuzenza Tongejiwe ambaye ni baba mzazi wa marehemu Salawa Tongejiwe Kuzenza
Katibu tawala wa wilaya Bwana Festo Chonya akiongea na wananchi wa kijiji cha Lyele
Afisa tarafa wa tarafa ya Chala Diana
Diwani wa kata ya Mkwamba Mh. Chiluba Mwandamo akiongea na wananchi wa kijiji cha Lyele
Mwenyekiti wa kijij cha Lyele Mh. Faustin Sindani akiongea na wananchi wa kijiji cha Lyele
Mwananchi wa kijiji cha Lyele Bwana Geofrey Matofali akiwasilisha maoni yake kwa mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda
Mfugaji wa kijiji cha Lyele Bwana Lyali Masanja akiwasilisha maoni yake kwa mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanada
Bonyeza kuitazama video ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanada akiongea na wakazi wa kijiji cha Tambaruka
Mwenyekiti wa kijiji cha Tambaruka akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda kijijini hapo
Afisa mtendaji wa kata ya Mkwamba Bwana Juvenary Mmanzi akiongea na wananchi wa kijiji cha Tambaruka
Afisa mtendaji wa kijiji Tambaruka Juliana Makasi akisoma taarifa ya maendeleo ya kijiji
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na wananchi wa kijiji cha Tambaruka
Wananchi wa kijiji cha Tambaruka wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda
WAKAZI wa kata ya Mkwamba wilayani nkasi mkoani rukwa wameiomba
serikali kuwapelekea huduma ya kituo cha afya na polisi katika kata hiyo
kutokana na changamoto kadhaa zinazowakabili.
Ombi hilo limetolewa na diwani wa kata hiyo ya Mkwamba
Chiluba Mwandamo kwa mkuu wa wilaya Nkasi Said Mtanda kwenye mikutano tofauti
aliyoifanya jana katika kata hiyo ya Mkwamba.
Amesema kata hiyo jiografia yake ni ngumu kiasi cha wananchi
wa eneo hilo kushindwa kupata huduma za haraka za kiafya baada ya kutokuwepo kituo
cha afya na kuazimikla kuifuata huduma hiyo mbali na wengine ulazimika kufariki
dunia kwa sababu ya kuchellewa kupata huduma hizo za kiafya kwa kwenda umbali
mrefu kufuata kituo cha afya kilipo.
Amesema kutokana na uhitaji wa huduma hiyo ya afya wananchi
wa kijiji cha tambaruka wamefyatua tofali 250,000 kama hakiba na kudai kuwa wao
wapo tayari kuanza kujenga kituo cha afya pale serikali itakaporidhia
Katika hatua nyingine diwani huyo aliomba katika kata hiyo
kijengwe kituo cha poisi hasa baaba ya eneo hilo kuwa na matukio mengi ya
kihalifu na kuwa suluhisho ni kuwa na kituo kidogo cha polisi katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya said Mtanda kwa upande wake amesema serikali
imekisikia kilio hicho na kuwa itakwenda kulifanyia kazi ombi hilo,huku
akipongeza jitihada za wananchi wa kijiji cha Tambaruka ambao wameanza
kufayatua matofali na kuwataka wananchi wengine katika vijiji vyao kuwa na
banki ya matofali ili kuweza kukabiliana na shughuli yoyote ya maendeleo
inayoitajika katika vyao
No comments:
Post a Comment