Tuesday, August 23, 2016

ZIARA YA WAZIRI MKUU MH KASSIM MAJALIWA WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiwa katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi kwa ajili ya mapokezi ya waziri mkuu


Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Rukwa wakiwa katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani wakiwa tayari kwa mapokezi ya waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa


Wanakikundi cha ngoma za asili wakitumbuiza katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi



Vijana wa skauti wakiwa katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi wakisubiri ujio wa Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa
Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akivishwa skafu na kijana wa skauti baada ya kuwasili katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi
Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa (kulia) akiwasili ikulu ndogo wilayani Nkasi (kushoto) ni mkuu wa mkoa wa rukwa Mh. Zellote Steven

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mh. Ally Mohamed  Keissy mbunge wa jimbo la Nkasi kaskazini baada ya kuwasili katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa (kulia) akiwasalimia wasanii wa ngoma za asili (kushoto) ni mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi
Waziri mkuu Mh. Majaliwa(katikati) akikagua mradi wa upanuzi wa bwawa la maji Mfiri (wa pili kutoka kushoto) ni mkuu wa mkoa wa rukwa Mh. Zellote Steven (anaefuata baada ya waziri mkuu) ni mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda (wa kwanza kutoka kulia) ni Mkurugenzi wa halmashauri bwana Julius Mseleche Kaondo

Mhandisi wa maji bwana Fransis Mapunda akisoma taarifa ya mradi wa upanuzi wa bwawa la maji Mfili baada ya waziri mkuu kufika katika mradi huo
Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya mradi wa upanuzi wa bwawa la maji Mfili
                                                                             
Wanafunzi wa chuo cha Mt. Bakhita wakiwa tayari kwa ajili ya mapokezi ya waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa ambaye alizindua wodi la wagonjwa katika hospitali teule ya wilaya NDDH

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akizindua wodi ya wagonjwa katika hospitali teule ya wilaya NDDH

     Waziri mkuu Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wilayani Nkasi mkoani      
      Rukwa
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh Said Mohamed Mtanda (mwenye miwani) akicheza na wanakwaya wa Sinai katika viwanja vya sabasaba (mwenye shati ya kijani) ni Mbunge wa Nkasi kusini na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Nkasi Mh. Desderius Mipata

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa ametoa maagizo kwa uongozi wa wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa kwa kuutaka uongozi huo kufanya zoezi la kuwaondoa watu wote wanaoishi katika kijiji cha Lyazumbi ambacho kipo ndani ya mita 500 ambazo zilitakiwa kuwa ndani ya hifadhi ya wanyama pori.

Agizo hilo limetolewa na waziri mkuu Mh. Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba kilichopo wilayani Nkasi,ambapo amesema wilaya hiyo inatakiwa kuwaondoa watu wote waliovamia hifadhi kwa kujenga au kufanya shughuli yoyote ndani ya hifadhi.



Na,Israel Mwaisaka,Nkasi
WAZIRI mkuu Majaliwa Kassimu Majaliwa   amesema kuwa serikali  inafanya uchunguzi wa kina ili kujua tatizo linalopelekea Mabweni  ya shule za Sekondari Nchini na kuwa kama kuna watu ambao ni chanzo  cha kuibuka kwa moto huo waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria .
Hayo ameyasema jana  kwenye mkutano wa hadhara mjini Namanyere wilayani Nkasi ambapo alidai kuwa serikali wakati ikiwa kwenye mikakati ya kuinua elimu Nchini kumejitokeza tatizo hilo la moto kiasi cha kuhisi kuwapo kwa hujuma.
Alisema kufuatia hari hiyo serikali imekaa na kuendelea kutafuta chanzo cha matukio hayo ya moto katika maeneo mbalimbali ya Nchi na kuwa sasa jeshi la polisi imeanza kuwakamata watu wanaohusishwa na kuchoma moto mabweni hayo kule mkoani  Arusha na kuwa kazi hiyo inaendelea na kuwa kama wakibainika watu hao serikali itawachukulia hatua kali ambazo hawataweza kusahau katika maisha yao yote.
Sambamba na hilo Waziri mkuu alidai kuwa katika maboresho ya elimu ambayo serikali imeendelea kuyafanya pia imejikita kumlinda mtoto wa kike dhidi ya vikwazo mbalimbali ambavyo wamekuwa wakivipata ambavyo vimekua vikipelekea  watoto wa kike kukatiza masomo yao
Alivitaja vikwazo hivyo kuwa mimba na kuwa sasa mtu yeyote atakayempa mimba mwanafunzi sheria ipo wazi na hawataachwa na kuwa sasa mwanaume aliyempa Mimba Mwanafunzi,aliyeoa mwanafunzi na wazazi waliopokea mali ya kumuoza mtoto  wao wote watashikitakiwa na kupewa adhabu hiyo
“katika kipindi hiki ambacho serikali serikali imejikita kuiboresha elimu hatutakubali wawepo baadhi ya watu wahalifu ambao kazi yao ni kuwakatisha masomo Wanafunzi kwa kuwapa mimba na kuwaoa wakiwa na umri mdogo ambao ilitakiwa wawepo shule”alisema Majaliwa
Lakini pia Majaliwa aliwataka Wananchi wanaovamia hifadhi kwenye vyanzo vya maji kutakiwa kuondoka haraka sana  kwani sheria inazoziinda hifadhi hizo ni kali mno na kuwa serikali haitawavumilia wale ote wanaovamia hifadhi hizo
Alisema serikali inatekeleza mradi mkubwa wa uchimbaji wa bwawa la maji la Mfili wilayani Nkasi ambalo litaghalimu Tshs,Bil.1 na kuwa haiwezekani fedha nyingi kiasi hicho zikatumika halafu wakawepo watu ambao wataharibu hifadhi hiyo ya chanzo cha maji na kupelekea  chanzo hicho kukauka
Kufuatia hari hiyo waziri mkuu huyo alimkabidhi sheria za hifadhi ya vyanzo vya maji mkuu wa wilaya Said Mtanda ili aweze kushirikiana na kamati yake ya ullinzi nla usalama katika kukabiliana na watu hao ambao ni waharibifu wa vyanzo vya maji
Alisema kuwa sheria iliyopo ni kali sana hivyo ili kuyaepuka matatizo hayo ni kutii sheria kwa kutovamia hifadhi hizo na kuwa haitakiwi kabisa kwa mtu kuwepo eneo la hifadhi ya chanzo cha maji wala kwenda kuongea eneo hilo kuwa kufanya hivyo ni kosa na adhabu yake kwa mujibu wa sheria ni kifungo cha miaka saba jela na faini ya Tshs,Milioni  70
Waziri mkuu katika ziara yake hapa wilayani Nkasi alipita kukagua mradi mkubwa wa bwawa a maji ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa wodi la wagonjwa katika  hospitali teule ya wilaya NDDH yenye uwezo wa kuwalaza  wagonjwa 72 kwa mkupuo mmoja
Majaliwa ameendelea na ziara katika mkoa Rukwa baada ya kupokelewa wilayani Nkasi akitokea wilaya ya Mlele mkoani Katavi

1 comment:

  1. Khasante kwa habari za ziara ya waziri MKUU .
    Mungu aendelee kukupigania MH DC NKASI

    ReplyDelete