Friday, August 19, 2016

MKUU WA WILAYA YA NKASI KUTATUA MGOGORO WA MADAI YA FEDHA

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda(kushoto) akipewa maelezo kutoka kwa msimamizi wa mradi bwana Peng
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na vibarua hao katika ofisi ya Mtendaji wa kijiji
Mkuu wa wilya ya Nkasi Mh.Said Mohamed Mtanda (katikati) akielekea katika ofisi ya mtendaji wa kijiji
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda ametoa siku moja kwa kampuni ya China Hunan Construction Engineering Group inayojenga barabara ya kutoka Kibaoni mkoani Katavi hadi kijiji cha Kanazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa wakiwa na Bwana Faustin Samwel(site for men) kufika katika ofisi za mkuu wa wilaya siku ya jumamosi saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kutoa muafaka wa kuwalipa madai yao vibarua wanaofanya kazi ya kuchimba mitaro ya kupitisha maji taka katika barabara hiyo.

Mkuu wa wilaya ya nkasi Mh. Mtanda ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kambi ya makandarasi hao na kufanya kikao cha pamoja kilichowakutanisha viongozi wa kampuni hiyo na Bwana Faustin Samwel(site for men)
Wakiongea mbele ya mkuu huyo wa wilaya baadhi ya vibarua hao wamemueleza mkuu huyo wa wilaya Mh.Mtanda kuwa wanamdai Bwana Faustin (site for men) shilingi milioni 7 kati ya milioni 12 walizokubaliana kwa ajili ya kutengeneza mitaro ya kupitisha maji taka kandokando ya barabara hiyo wenye urefu wa mita 750.

Aidha katika kikao hicho Bwana Peng ambaye ni msimamizi wa mradi huo  alisema kampuni ilimpatia kazi ya usimamizi mwangalizi wa mradi huo(site for men) bwana Faustin yakutengeneza mifereji hiyo kwa mapatano ya shilingi milioni 30 ambapo hadi sasa tayari wamelipa shilingi milioni 5.
"Mkuu kampuni inao waangalizi wake wa mradi kwa ajili ya kurahisisha shughuli ya ujenzi ambapo kampuni yetu ilimpatia jukumu la usimamizi wa ujenzi wa mifereji hiyo Faustin ambaye nae anadaiwa alitumia fedha hizo kwa kumpatia kaka yake ajiendeleze kibiashara" alisema Peng

Kutokana na maelezo hayo ndipo mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh.Said Mohamed Mtanda akatoa muda kwa bwana Faustin kuhakikisha anakamilisha malipo yote kwa vibarua hao huku akiwataka viongozi wa kampuni hiyo ya ujenzi China Hunan Construction Engineering Group kufika katika ofisi yake na kutoa maelezo ya kuchelewesha malipo.

1 comment: