Vibarua wakiwa katika ofisi ya mtendaji |
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akisikiliza kwa umakini maelezo ya uongozi wa kampuni ya China Hunan Construction Group |
Mkuu wa wilaya ya nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda baada yakutoa siku 3 kwa kampuni ya China Hunan Construction Group iwe imewalipa vibarua kiasi cha shilingi milioni 8.7 katika makubaliano yaliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya mapema leo, kabla yakumalizika kikao hicho bwana Peng ambaye ni msimanizi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kibaoni hadi kijiji cha Kanazi aliahidi kulipa fedha hiyo masaa 4 mara baada yakumalizika kwa kikao hicho.
Mkuu huyo wa wilaya ya Nkasi Mh. Mtanda ili kuhakikisha fedha hiyo inatolewa kwa wakati muafaka baada ya masaa tajwa alifika katika kambi ya makandarasi hao na kuwataka kutoa hiyo fedha mara moja kwa ajili ya malipo ya vibarua hao.
Akiongea na msimamizi wa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo bwana Peng, mkuu wa wilaya ya nkasi Mh. Mtanda alisema wao kama kampuni hawapaswi kutoa kazi kwa mtu au kampuni isiyo na usajiri, Hivyo amewataka kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao kwenye kampuni hiyo.
Aidha mwangalizi wa mradi huo(site for men) bwana Faustin Samwel alikabidhiwa kiasi cha shilingi miliioni 8.7 mbele ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Mtanda kwa ajili ya malipo ya vibarua hao,
Akizungumza na vibarua hao katika ofisi ya mtendaji wa kata hiyo mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Mtanda aliwataka kufanya kazi kwa mikataba pia wapewe vitambulisho vya muda (Temporary Job Card).
No comments:
Post a Comment