Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akisikiliza hoja za Maafisa watendaji wa kata, vijiji pamoja na wakuu wa idara mbalimbali za Halmashauri |
Katibu tawala wa wilaya Bwana Festo Chonya akitoa ufafanuzi wa hoja zilizotelewa na Maafisa watendaji wa kata na vijiji wilayani Nkasi |
SERIKALI
wilayanil Nkasi mkoani Rukwa imesema kuwa mkakati wake mkubwa kwa sasa ni
kuhakikisha kuwa madawati 3337 yaliyobaki kukamilika ili kuondoa kabisa tatizo
la madawati wilayani hapa inakamilika ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.
Akizungumza na
wakuu wa idara,vitengo,watendaji wa kata na vijiji katika mkutano wao wa kikazi
mkuu wa wilaya Nkasi Said Mtanda amesema huo ndiyo mkakati wa wilaya na kumtaka
kila mmoja katika nafasi yake kuhakikisha kuwa anajiandaa kisaikolojia katika
kuhakikisha kuwa zoezi la madawati linakamilika ndani ya mwezi mmoja kuanzia
sasa
Amesema katika
mpango huo halmashauri ya wilaya itatengeneza madawati 2500 na kila kijiji kimepewa jukumu la kutengeneza madawati matano
na kuwa watamchukulia hatua kali mtu yoyote atakayekwamisha mpango huo na
kutaka serikali za vijiji kuhakikisha kuwa madawati ndani ya mwezi mmoja madawati
hayo yawe yamekamilika.
Lakini pia
amedai kuwa mkakati wa serikali sasa ni kuwaondoa watumishi wote wa serikali ambao ni mizigo ambao wanalewa
wakati wa kazi na kuwa serikali lengo lake ni kuwaondoa wote watumishi wa namna
hiyo.
Lakini pia
mkuu huyo wa wilaya amesikitishwa na kasi ya mauaji inayoendelea willayani
Nkasi kwa sasal na kuwa ipo haja sasa jambo hilo kuangaliwa upya na kuifanya wilaya
Nkasi kuwa eneo salama.
Kwa upande
wake mkurugenzi mtendaji wa wilaya Julius Mseleche Kaondo amewataka watendaji
hao wa serikali kuzingatia yale yote waliyoelekezwa huku kubwa ikiwa ni suala
zima la makusanyo ya halmashauri
Mkutano huo
pia uliwashikirisha wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama ambao nao pia
walitoa mada mbalimbali
No comments:
Post a Comment