Thursday, October 27, 2016

DC ATOA SIKU 10 KWA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI BOMBA MATALA

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na wananchi wa kijiji cha Matala 











Diwani wa kata ya Mtenga Mh. Pankras Maliyatabu akiongea na wananchi wa kijiji cha Matala
Afisa mtendaji wa kata ya Mtenga Bwana Joshua Mwimanzi akiwahimiza wananchi wa kijiji cha Matala kujikita zaidi katika shughuli za maendeleo

Afisa tarafa ya Namanyere Bwana Kassim Abdul akitambulisha viongozi wa serikali walioambatana na mkuu wa wilaya katika ziara 
Afisa mtendaji wa kijiji cha Matala Bwana Revocatus Tinga akijibu maswali yaliyo ulizwa na mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda
Mhandisi wa maji Bwana Francis Mapunda akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa maji kijiji cha Matala
Mkandarasi wa mradi wa maji kijiji cha Matala Bwana Jofrey Godfrey akifanya mawasiliano na mmoja wa wahusika katika ujenzi wa mradi

 Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akiongea na wananchi wa kijiji cha Matala katika mkutano wa hadhara

Bwana Silvanus Malisela mkazi wa kijiji cha Matala akiuliza swali juu ya ubovu wa miundo mbinu ya barabara inayotoka kijiji cha Mtenga mpaka katika kijiji cha Matala
Bwana Claudio Kastiko mkazi wa kijiji cha Matala akiomba ufafanuzi kuhusu wafugaji wafugaji wanao kaidi agizo la serikali


 Bi Lishada Melimeli mkazi wa kijiji cha Matala akihoji juu ya fedha za mikopo ya vikundi vya akina mama zilizo takiwa kutolewa kwa mujibu wa ahadi ya Mh. Rais Magufuli




Bonyeza ili kutazama video ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akiwahoji Mhandisi wa maji na Mkandarasi wa mradi katika mkutano wa hadhara


Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda ametoa siku 10 kwa mkandarasi wa mradi wa maji bomba Bwana Jofrey Godfrey na Mhandisi wa maji Bwana Francis Mapunda kukamilisha mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Matala wilayani Nkasi mkoani Rukwa
Akiongea alhamisi hii katika mkutano wa hadhara mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda amesema mradi huo umekuwa ukisuasua muda mrefu bila mafanikio na kuwataka kuukamilisha mradi huo ndani ya mwezi mmoja na kuahidi kutembelea mradi huo baada ya siku 10 ambapo mkandarasi wa mradi huo amedai kutumia siku 7 kukamilisha mfumo wa umeme jua kwa ajili ya uendeshaji wa mashine ya kuvuta maji
Amesema pamoja na kuwepo fedha kwenye akaunti kwa ajili ya mradi huo bado utekelezaji wa mradi huo umekuwa ukitekelezwa chini ya kiwango na mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi milioni 422 na mpaka sasa mkandarasi tayari ameshalipwa shilingi milioni 258
Akiwa katika ziara ya ukaguzi wa mradi wa maji mkuu huyo wa wilaya ya Nkasi Mh. Mtanda ametumia ziara hiyo kutoa Jenereta katika shule ya msingi Matala ili kuwapa wanafunzi uwezo wa kujisomea wakati wa usiku


Thursday, September 29, 2016

DC AHUDHURIA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI KAZOVU




Bonyeza ili kutazama video ya Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda akiwa katika mahafali ya kidato cha nne Shule ya sekondari Kazovu
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda (katikati) akitembelea mazingira ya Shule ya sekondari Kazovu


Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda (katikati) na kulia ni Kaimu Afisa tawala wa wilaya Bwana Kassim Abdul (kushoto) ni Mkuu wa Shule ya sekondari Kazovu Bwana  Elieza Dononda

Mkuu wa shule ya sekondari Kazovu Bwana Elieza Dononda akisoma ratiba ya mahafali ya kidato cha nne

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Kazovu pamoja na wageni waalikwa katika mahafali ya kidato cha nne
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda akipiga picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Kazovu na wanafunzi wa kidato cha nne
Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kazovu
Mkuu wa shule ya sekondari Kazovu na Makamu wa shule wakisoma taarifa ya shule

Wanafunzi wa kidato cha nne wakisoma taarifa ya Wanafunzi wa shule ya sekondari Kazovu

Kwaya ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kazovu


Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed mtanda akigawa vyeti kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika mahafali yaliyofanyika katika shule ya sekondari Kazovu
Wageni waalikwa wakiwa katika mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari Kazovu
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda amewataka walimu wa shule ya sekonadari Kazovu iliopo kijiji cha Kazovu Wilayani Nkasi mkoani Rukwa kuwapa kipaumbele kimasomo wanafunzi wa kike ili waweze kuwa viongozi wa baadae.
Ameyasema hayo mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanada jumatano ya wiki hii katika mahafali ya kidato cha nne yaliyofanyika katika shule ya sekondari Kazovu ambapo amezungumzia changamoto zinazo wakabili watoto wa kike ni pamoja na kutopewa kipaumbele katika masomo mashuleni
Aidha mkuu huyo wa wilaya aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne ambayo ni mahafali ya pili kwa shule hiyo tangu ilipofunguliwa mwaka 2009 kupitia arambee iliyofanyika katika mahafali hayo aliweza kuchangia kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya maendeleo ya shule hiyo
Kupitia mahafali hayo mkuu huyo wa wilaya Mh Mtanda amekemea kuwapo kwa mahusiano yanayo wahusisha Walimu na wanafunzi katika shule hiyo na kwamba atafanya uchunguzi ili kuweza kuwabaini Walimu wenye tabia hiyo na kuwachukulia hatua za kinidhamu pia kuwachukulia hatua wazazi wanao waoza wanafunzi kabla ya kumaliza masomo
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Bwana Elieza Dononda amewataka wananchi wa kijiji cha Kazovu kutoa ushirikiano katika maendeleo ya shule hiyo ambapo wazazi wa kata hiyo wanashiriki katika ujenzi wa shule kwa asilimia 20% kati ya asilimia 100%  na wanafunzi wa shule hiyo wanaotokea kwenye kata hiyo wanapunguzo la ada
Katika taarifa ya shule hiyo iliyosomwa na mkuu wa shule Bwana Elieza na makamu wake Pascharia Joseph wamesema mnamo mwaka 2015 shule imeweza kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya kidato cha nne kimkoa




Wednesday, September 28, 2016

DC AWAPA SIKU 7 WANANCHI WA KIJIJI CHA LYAZUMBI KUONDOKA NDANI YA HIFADHI



Bonyeza ili kutazama video ya Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akitoa siku 7 kwa wananchi wa kijiji cha Lyazumbi walioweka makazi katika hifadhi ya Lwafi na kutoa agizo kwa wananchi wengine kusitisha ujenzi wa majengo mapya katika kijiji hicho



Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akitoa siku 7 kwa wanachi wa kijiji cha Lyazumbi kuhama katika eneo la hifadhi


Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiwa katika mkutano wa hadhara kijiji cha Lyazumbi
Afisa tawala wilaya ya Nkasi Bwana Festo Chonya akiwasisitiza wananchi wa kijiji cha Lyazumbi kutii agizo la Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda

Mwenyekiti wa kijiji cha Lyazumbi Mh. Iddi Lehani
Afisa mtendaji wa kijiji cha Lyazumbi Elizabeth Felix akisoma taarifa ya maendeleo ya kijiji

Diwani wa kata ya Paramawe Mh. January Kakuwi akimpongeza Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda baada ya kuonyesha uvumilivu kwa baadhi ya vijana wa kijiji cha Lyazumbi ambao wamekuwa sio waadilifu
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akionea na wananchi wa kijiji cha Lyazumbi

Wananchi wa kijiji cha Lyazumbi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda

Moja kati ya majengo yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya Lwafi


Tuesday, September 27, 2016

DC KUTATUA MIGOGORO KATI YA WATUMISHI WA SERIKALI NA UONGOZI WA VIJIJI KATA YA KALA





Bonyeza ili kutazama video ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na wakazi wa kata ya Kala tarafa ya Wampembe kuhusiana na masuala mbalimbali wanayotakiwa kuzingatia wananchi pamoja na viongozi wao wa vijiji, kata  hadi tarafa


Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na watumishi wa serikali pamoja na viongozi wa serikali za vijiji katika kikao cha ndani

Mratibu elimu kata Bwana Alan akisoma taarifa ya kata ya Kala mara baada ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda kuwasili kwenye kata hiyo

Afisa mtendaji wa kata ya Kala Bwana Privev Mwasile akijibu swali lililouzwa na mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda

Kaimu afisa tarafa ya Wampembe Bwana Erasto Widambe

Afisa mtendaji wa kijiji cha Kilambo cha mkolechi Bwana Meshack Chakupewa akijibu hoja iliyotokana na mgogoro uliozuka kati yake na Mwenyekiti wa kijiji hicho

Msimamizi wa kituo cha afya Kala Bwana Nashon Omolo akizungumzia changamoto za usafiri kwa wagonjwa katika kata ya Kala

Mwenyekiti wa kijiji cha Kala Mh.Abdallah Said

Diwani kata ya Kala Mh.Thadeo Kisoli

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda (katikati) akiwa katika mkutano wa hadhara kata ya Kala

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na wananchia wa kata ya Kala katika mkutano wa hadhara

Bwana Julius Vilimani mkazi wa kata ya Kala akizungumzia juu ya mradi wa maji ambao haujakamilika tangu mwaka 2012

Wakazi wa kata ya Kala wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda katika mkutano wa hadhara

Bwana Jordan Kapondo mkazi wa kata ya Kala akitoa ombi la uvuvi wa samaki kwa kutumia taa za Sola kwa mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda

Afisa Uvuvi kata ya Kala Bwana Frank akitoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na sheria za uvuvi

Mwenyekiti wa kijiji cha Mpasa Mh. Amos Chipeta akitoa ombi la ujenzi wa kituo cha afya badala ya Zahanati huku akisisitiza kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha polisi
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda (kushoto) akimuuliza maswali mwenyekiti wa kijiji cha Mpasa
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiwa katika kikao kilifanyika kwa aijili ya kutatua mgogoro kati ya mtendaji wa kijiji cha Kilambo cha mkolechi na serikali ya kijiji hicho

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea atembelea daraja la miti ambalo limekuwa kilio kikubwa kwa wananchi wa kata ya Kala ambapo wafanzi wengi wamekuwa wakiangusha mikoba ya madaftari na viatu wakati wa kuvuka katika daraja hilo ambalo pia ni kiunganishi kati ya kata ya Kala na kata ya Wampembe

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda (kulia) akiongea na mkuu wa idara ya Mifugo na Uvuvi katika chumba cha kuhifadhia vifaa mbali mbali vinavyotumika katika uvuvi haramu

Afisa uvuvi kata ya Kala Bwana Frank akionyesha nyavu haramu

Taa zinazotumika katika uvuvi uliopigwa marufuku kisheria

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na wananchi wa kijiji cha King'ombe
Wananchi wa kijiji cha king'ombe wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda atembelea Mradi wa maji uliojengwa chini ya kiwango katika kijiji cha King'ombe

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na Mwenyekiti wa kijiji cha King'ombe katika eneo la mradi
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda (wa pili kutoka kulia) akiondoka katika eneo la mradi wa maji kijiji cha King'ombe kata ya Kala tarafa ya Wambembe baada ya kukagua mradi huo uliojengwa chini ya kiwango ambapo uongozi wa serikali ya kijiji umebainisha kuwekwa bomba zisizofaa kwa ajili ya kusafirisha maji yanayotoka kilometa kadhaa mpaka kufika katika chanzo cha maji hayo