Tuesday, August 30, 2016

DC AHAMASISHA UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANI WILAYANI NKASI

 Bonyeza ili uweze kutazama video ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na  watendaji wa kata


Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akisisitiza juu ya ukusanyaji wa mapato ya ndani
                   
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiwasikiliza watendaji wa kata kwa umakini


Watendaji wa kata wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda katika ukumbi wa Halmashauri wilayani Nkasi
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi Julius Mseleche Kaondo akitoa ufafanuzi juu ya ukusanyaji mapato ya ndani kwa watendaji wa kata
                                                                              
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mh. Zeno Sumuni Mwanakulya


Afisa mtendaji wa kata ya Majengo wilayani Nkasi Rock Msalange akizungumzia juu ya changamoto zilizopo katika ukusanyaji mapato



MKUU wa wilaya Nkasi Said Mohammed Mtanda amesema kuwa uwezekano wa halmashauri ya wilaya Nkasi kuvuka malengo yake ya ukusanyajli wa mapato inawezekana klamla watendaji watabadilika na kuafanya kazi kwa mazingira ya uadillifu
Akizungumza na maafisa watendaji wa kata kwenye kikao chao cha kazi mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa amefanya ziara za kushitukiza katika maeneo mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato na kubaini mianya mingi inayoikosesha mapato halmashauri na kuwa sasa ni wakati wa kujituma kufanya kazi na atakayezembea  kama uzembe unaoonekana sasa miongoni mwa watendaji hawatavumiliana bali hatua stahiki zitachukuliwa.
Amesema moja ya dhambi kubwa kwa mtendaji wa serikali ni pale mtendaji anapovunja sheria na kupelekea  kupotea kwa mapato ya hamashauri na kuwa mtendaji wa namna hiyo ni lazima achukuliwe hatua stahiki za kinidhamu.
Mkuu huyo wa wilaya ametaka  wakuu wa idara mbalimbali za halmashauri kufanya ziara za kushitukiza katika maeneo mbalimbali ya wilaya na kufanya  ukaguzi kwa watumishi walio chini yao na kuwa kwa kufanya hivyo watabaini mambo kadha wa kadha na kuweza kuyafanyia kazi baadhi ya mambo wanayoyakuta pale kama hayaendi vizuri na kuchukua hatua za haraka pale pale
Na kudai kuwa ameagiza watendaji wa kata na vijiji  kuhakikisha kuwa wanawakamata wahamiaji haramu waliovamia katika nchi hii hususani mwambao mwa ziwa Tanganyika ili kuleta utengamavu na utulivu katika nchi hii.
Mkurugenzi mtendaji Julius Mseleche Kaondo kwa upande wake amesema kuwa kikao hicho kimelenga kukumbushana mambo mengi ya msingi na kuwa mengi aliyoyasema mkuu wa wilaya ndiyo wamekua wakikumbusha na kila wakati na kuwa kila jambo ni muhimu kulifanyia kazi

                                                                                    

Tuesday, August 23, 2016

ZIARA YA WAZIRI MKUU MH KASSIM MAJALIWA WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiwa katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi kwa ajili ya mapokezi ya waziri mkuu


Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Rukwa wakiwa katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani wakiwa tayari kwa mapokezi ya waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa


Wanakikundi cha ngoma za asili wakitumbuiza katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi



Vijana wa skauti wakiwa katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi wakisubiri ujio wa Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa
Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akivishwa skafu na kijana wa skauti baada ya kuwasili katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi
Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa (kulia) akiwasili ikulu ndogo wilayani Nkasi (kushoto) ni mkuu wa mkoa wa rukwa Mh. Zellote Steven

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mh. Ally Mohamed  Keissy mbunge wa jimbo la Nkasi kaskazini baada ya kuwasili katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa (kulia) akiwasalimia wasanii wa ngoma za asili (kushoto) ni mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda katika viwanja vya ikulu ndogo wilayani Nkasi
Waziri mkuu Mh. Majaliwa(katikati) akikagua mradi wa upanuzi wa bwawa la maji Mfiri (wa pili kutoka kushoto) ni mkuu wa mkoa wa rukwa Mh. Zellote Steven (anaefuata baada ya waziri mkuu) ni mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda (wa kwanza kutoka kulia) ni Mkurugenzi wa halmashauri bwana Julius Mseleche Kaondo

Mhandisi wa maji bwana Fransis Mapunda akisoma taarifa ya mradi wa upanuzi wa bwawa la maji Mfili baada ya waziri mkuu kufika katika mradi huo
Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya mradi wa upanuzi wa bwawa la maji Mfili
                                                                             
Wanafunzi wa chuo cha Mt. Bakhita wakiwa tayari kwa ajili ya mapokezi ya waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa ambaye alizindua wodi la wagonjwa katika hospitali teule ya wilaya NDDH

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akizindua wodi ya wagonjwa katika hospitali teule ya wilaya NDDH

     Waziri mkuu Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wilayani Nkasi mkoani      
      Rukwa
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh Said Mohamed Mtanda (mwenye miwani) akicheza na wanakwaya wa Sinai katika viwanja vya sabasaba (mwenye shati ya kijani) ni Mbunge wa Nkasi kusini na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Nkasi Mh. Desderius Mipata

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa ametoa maagizo kwa uongozi wa wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa kwa kuutaka uongozi huo kufanya zoezi la kuwaondoa watu wote wanaoishi katika kijiji cha Lyazumbi ambacho kipo ndani ya mita 500 ambazo zilitakiwa kuwa ndani ya hifadhi ya wanyama pori.

Agizo hilo limetolewa na waziri mkuu Mh. Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba kilichopo wilayani Nkasi,ambapo amesema wilaya hiyo inatakiwa kuwaondoa watu wote waliovamia hifadhi kwa kujenga au kufanya shughuli yoyote ndani ya hifadhi.



Na,Israel Mwaisaka,Nkasi
WAZIRI mkuu Majaliwa Kassimu Majaliwa   amesema kuwa serikali  inafanya uchunguzi wa kina ili kujua tatizo linalopelekea Mabweni  ya shule za Sekondari Nchini na kuwa kama kuna watu ambao ni chanzo  cha kuibuka kwa moto huo waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria .
Hayo ameyasema jana  kwenye mkutano wa hadhara mjini Namanyere wilayani Nkasi ambapo alidai kuwa serikali wakati ikiwa kwenye mikakati ya kuinua elimu Nchini kumejitokeza tatizo hilo la moto kiasi cha kuhisi kuwapo kwa hujuma.
Alisema kufuatia hari hiyo serikali imekaa na kuendelea kutafuta chanzo cha matukio hayo ya moto katika maeneo mbalimbali ya Nchi na kuwa sasa jeshi la polisi imeanza kuwakamata watu wanaohusishwa na kuchoma moto mabweni hayo kule mkoani  Arusha na kuwa kazi hiyo inaendelea na kuwa kama wakibainika watu hao serikali itawachukulia hatua kali ambazo hawataweza kusahau katika maisha yao yote.
Sambamba na hilo Waziri mkuu alidai kuwa katika maboresho ya elimu ambayo serikali imeendelea kuyafanya pia imejikita kumlinda mtoto wa kike dhidi ya vikwazo mbalimbali ambavyo wamekuwa wakivipata ambavyo vimekua vikipelekea  watoto wa kike kukatiza masomo yao
Alivitaja vikwazo hivyo kuwa mimba na kuwa sasa mtu yeyote atakayempa mimba mwanafunzi sheria ipo wazi na hawataachwa na kuwa sasa mwanaume aliyempa Mimba Mwanafunzi,aliyeoa mwanafunzi na wazazi waliopokea mali ya kumuoza mtoto  wao wote watashikitakiwa na kupewa adhabu hiyo
“katika kipindi hiki ambacho serikali serikali imejikita kuiboresha elimu hatutakubali wawepo baadhi ya watu wahalifu ambao kazi yao ni kuwakatisha masomo Wanafunzi kwa kuwapa mimba na kuwaoa wakiwa na umri mdogo ambao ilitakiwa wawepo shule”alisema Majaliwa
Lakini pia Majaliwa aliwataka Wananchi wanaovamia hifadhi kwenye vyanzo vya maji kutakiwa kuondoka haraka sana  kwani sheria inazoziinda hifadhi hizo ni kali mno na kuwa serikali haitawavumilia wale ote wanaovamia hifadhi hizo
Alisema serikali inatekeleza mradi mkubwa wa uchimbaji wa bwawa la maji la Mfili wilayani Nkasi ambalo litaghalimu Tshs,Bil.1 na kuwa haiwezekani fedha nyingi kiasi hicho zikatumika halafu wakawepo watu ambao wataharibu hifadhi hiyo ya chanzo cha maji na kupelekea  chanzo hicho kukauka
Kufuatia hari hiyo waziri mkuu huyo alimkabidhi sheria za hifadhi ya vyanzo vya maji mkuu wa wilaya Said Mtanda ili aweze kushirikiana na kamati yake ya ullinzi nla usalama katika kukabiliana na watu hao ambao ni waharibifu wa vyanzo vya maji
Alisema kuwa sheria iliyopo ni kali sana hivyo ili kuyaepuka matatizo hayo ni kutii sheria kwa kutovamia hifadhi hizo na kuwa haitakiwi kabisa kwa mtu kuwepo eneo la hifadhi ya chanzo cha maji wala kwenda kuongea eneo hilo kuwa kufanya hivyo ni kosa na adhabu yake kwa mujibu wa sheria ni kifungo cha miaka saba jela na faini ya Tshs,Milioni  70
Waziri mkuu katika ziara yake hapa wilayani Nkasi alipita kukagua mradi mkubwa wa bwawa a maji ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa wodi la wagonjwa katika  hospitali teule ya wilaya NDDH yenye uwezo wa kuwalaza  wagonjwa 72 kwa mkupuo mmoja
Majaliwa ameendelea na ziara katika mkoa Rukwa baada ya kupokelewa wilayani Nkasi akitokea wilaya ya Mlele mkoani Katavi

Saturday, August 20, 2016

HATIMAYE KAMPUNI YA CHINA HUNAN CONSTRUCTION ENGINEERING GROUP YATEKELEZA AGIZO LA MKUU WA WILAYA

Bonyeza kuitazama video ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akitoa agizo kwa kampuni ya China Hunan Construction Engineering Group
 

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda(kulia) akiwapatia fedha vibarua katika ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata
Vibarua wakiwa katika ofisi ya mtendaji
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda (katikati) na (kulia) ni uongozi wa China Hunan Construction Group (kushoto) ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakijadili kwa pamoja kuhusiana na madai ya vibarua
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akisikiliza kwa umakini maelezo ya uongozi wa kampuni ya China Hunan Construction Group














Mkuu wa wilaya ya nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda baada yakutoa siku 3 kwa kampuni ya China Hunan Construction Group iwe imewalipa vibarua kiasi cha shilingi milioni 8.7 katika makubaliano yaliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya mapema leo, kabla yakumalizika kikao hicho bwana Peng ambaye ni msimanizi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kibaoni hadi kijiji cha Kanazi aliahidi kulipa fedha hiyo masaa 4 mara baada yakumalizika kwa kikao hicho.

Mkuu huyo wa wilaya ya Nkasi Mh. Mtanda ili kuhakikisha fedha hiyo inatolewa kwa wakati muafaka baada ya masaa tajwa alifika katika kambi ya makandarasi hao na kuwataka kutoa hiyo fedha mara moja kwa ajili ya malipo ya vibarua hao.
Akiongea na msimamizi wa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo bwana Peng, mkuu wa wilaya ya nkasi Mh. Mtanda alisema wao kama kampuni hawapaswi kutoa kazi kwa mtu au kampuni isiyo na usajiri, Hivyo amewataka kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao kwenye kampuni hiyo.

Aidha mwangalizi wa mradi huo(site for men) bwana Faustin Samwel alikabidhiwa kiasi cha shilingi miliioni 8.7 mbele ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Mtanda kwa ajili ya malipo ya vibarua hao,
Akizungumza na vibarua hao katika ofisi ya mtendaji wa kata hiyo mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Mtanda aliwataka kufanya kazi kwa mikataba pia wapewe vitambulisho vya muda (Temporary Job Card).

Friday, August 19, 2016

MKUU WA WILAYA YA NKASI KUTATUA MGOGORO WA MADAI YA FEDHA

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda(kushoto) akipewa maelezo kutoka kwa msimamizi wa mradi bwana Peng
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akiongea na vibarua hao katika ofisi ya Mtendaji wa kijiji
Mkuu wa wilya ya Nkasi Mh.Said Mohamed Mtanda (katikati) akielekea katika ofisi ya mtendaji wa kijiji
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda ametoa siku moja kwa kampuni ya China Hunan Construction Engineering Group inayojenga barabara ya kutoka Kibaoni mkoani Katavi hadi kijiji cha Kanazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa wakiwa na Bwana Faustin Samwel(site for men) kufika katika ofisi za mkuu wa wilaya siku ya jumamosi saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kutoa muafaka wa kuwalipa madai yao vibarua wanaofanya kazi ya kuchimba mitaro ya kupitisha maji taka katika barabara hiyo.

Mkuu wa wilaya ya nkasi Mh. Mtanda ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kambi ya makandarasi hao na kufanya kikao cha pamoja kilichowakutanisha viongozi wa kampuni hiyo na Bwana Faustin Samwel(site for men)
Wakiongea mbele ya mkuu huyo wa wilaya baadhi ya vibarua hao wamemueleza mkuu huyo wa wilaya Mh.Mtanda kuwa wanamdai Bwana Faustin (site for men) shilingi milioni 7 kati ya milioni 12 walizokubaliana kwa ajili ya kutengeneza mitaro ya kupitisha maji taka kandokando ya barabara hiyo wenye urefu wa mita 750.

Aidha katika kikao hicho Bwana Peng ambaye ni msimamizi wa mradi huo  alisema kampuni ilimpatia kazi ya usimamizi mwangalizi wa mradi huo(site for men) bwana Faustin yakutengeneza mifereji hiyo kwa mapatano ya shilingi milioni 30 ambapo hadi sasa tayari wamelipa shilingi milioni 5.
"Mkuu kampuni inao waangalizi wake wa mradi kwa ajili ya kurahisisha shughuli ya ujenzi ambapo kampuni yetu ilimpatia jukumu la usimamizi wa ujenzi wa mifereji hiyo Faustin ambaye nae anadaiwa alitumia fedha hizo kwa kumpatia kaka yake ajiendeleze kibiashara" alisema Peng

Kutokana na maelezo hayo ndipo mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh.Said Mohamed Mtanda akatoa muda kwa bwana Faustin kuhakikisha anakamilisha malipo yote kwa vibarua hao huku akiwataka viongozi wa kampuni hiyo ya ujenzi China Hunan Construction Engineering Group kufika katika ofisi yake na kutoa maelezo ya kuchelewesha malipo.

Thursday, August 18, 2016

MKUU WA WILAYA ATOA SABUNI KWA WAFUNGWA

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akitoa zawadi ya sabuni kwa wafungwa wa gereza la Kitete
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda ametoa zawadi ya Sabuni kwa wafungwa wa gereza la Kitete lililopo wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
Akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kikazi wilayani humo Mh.Said Mohamed Mtanda aliweza kusalimiana na wafungwa hao na kisha kuwapatia zawadi ya boksi za Sabuni.

MKUU WA WILAYA AANZISHA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda akihakiki vyeti vyake ofisini kwake
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda ameanza leo zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi 20 wa ofisi ya mkuu wa wilaya na halmashauri kwa kuanza na yeye mwenyewe.
Akiongelea sababu ya kuanza kwa uhakiki huo mkuu wa wilaya ya Nkasi Said Mtanda amesema amelazimika kuanza ukaguzi katika ofisi yake ili kutoa mfano kwa idara nyingine kuanza mara moja uhakiki wa vyeti vya taaluma kwa watumishi wake.
Katika uhakiki huo pia kumefanyika uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa kwa watumishi wa ofisi ya mkuu huyo wa wilaya.

BRIGADIA GENERAL E.F. MANGOLE AKAGUA ENEO LA UJENZI WA KIKOSI CHA JESHI

General E.F MANGOLE akitia saini katika kitabu cha wageni ofisi ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda
Mkurugenzi wa matumizi ya ardhi wa jeshi la wananchi Tanzania, Brigadia General E.F MANGOLE akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa kwa ajili ya kukagua matumizi na maeneo ya ardhi ya jeshi hilo wilayani humo.
Akiwa wilayani Nkasi mkoani Rukwa Brigadia General Mangole alitembelea maeneo ya ardhi ya jeshi hilo akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda

Tuesday, August 16, 2016

MKUU WA WILAYA ATEMBELEA MNADA, AZUNGUMZA NA BAADHI YA WAFANYA BIASHARA

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohammed Mtanda akizungumza na mfanya biashara ya ng'ombe ikiwa ni pamoja na kukagua risiti na vibali vya kusafirishia ng'ombe hao
                                        
Mkuu wa wilaya Mh Said Mtanda akikagua risiti na vibali vya wafanya biashara ya Ng'ombe
Mkuu wa wilaya Mh. Said Mtanda akitoa maelekezo kwa mfanya biashara ya samaki na dagaa Mr. Lameki (kulia) amabaye alitoa malalamiko kwa mkuu wa wilaya huyo.

Mkuu wa wilaya akisalimaiana na wafanyakazi wa kampuni ya simu waliokuwa wakitoa huduma zao mnadani hapo
Mkuu wa wilaya Mh. Said Mtanda (kulia) akizungumza na mfanya biashara ya nguo za mitumba mnadani hapo

Sunday, August 14, 2016

ZIARA YA NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) WILAYANI NKASI SELEMAN JAFFO


 
Mkuu wa wilaya ya nkasi Mh. Said Mohammed Mtanda akimsomea taarifa ya wilaya naibu Waziri wa TAMISEMI Jaffo
Watumishi wa halmashauri ya wilaya nkasi wakimsikiliza Waziri wa TAMISENI jaffo wakati akizungumza nao baada ya kutoka kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Nkasi katika ziara yake ya siku moja
Waziri Jaffo akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi
Waziri wa tamisemi Suleiman Jaffo akitoa maelekezo kwa mkuu wa Wilaya na katibu tawala wa Wilaya juu ya ziara yake mara tu baada ya kusaini kitabu cha wageni
Waziri Jaffo akitizama bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nkomolo wilayani Nkasi ambalo siku ya hivi karibuni liliungua moto
wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Nkasi wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa TAMISEM seleman Jaffo,Kushoto waliokaa kwenye kiti ni,mbunge wa jimbo la Nkasi kasikazini Ally Kessy,wa pili ni Mkuu wa wilaya Nkasi said Mtanda na wa Mwisho ni mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri ya wilaya julius Mseleche Kaondo

Saturday, August 13, 2016

BWENI LA SHULE YA SEKONDARI LATEKETEA KWA MOTO




BWENI la Wanafunzi wa shule ya sekondari  ya Nkomolo wilayani Nkasi mkoani Rukwa limeteketea kwa moto huku wanafunzi wakinusurika.
Moto huo umetokea jana majira ya saa mbili usiku wakati wanafunzi hao walipokuwa darasani wakijisomea huku bweni na vifaa vilivyomo vyote kuteketea kwa moto
Akizungumza jana mkuu wa wilaya ya Nkasi  Said Mohammed Mtanda alisema kuwa baada ya moto huo kuwaka katika bweni hilo wananchi walijitokeza kwa wingi kuanza kuuzima moto huo ingawa juhudi hizo hazikuzaa matunda .
Alisema kuwa  uwezo wa bweni hilo ni kuchukua wanafunzi  48 lakini wanafunzi waliokuwa wakilitumia bweni walikua ni 14 ambapo wengine walihamishiwa mabweni mengine kabla ya moto huo kutokea.
Mkuu huyo wa wilaya alidai kuwa  serikali baada ya uchunguzi wake imebaini kuwa moto huo umetokea baada ya Chemry moja ndani ya bweni hilo kupasuka.
Alidai kuwa kimsingi moto huo umetokea kwa sababu za uzembe kwa waalimu wa shule hiyo kwa kutumia taa ambapo serikali imekataza matumizi ya taa na mishumaa kwenye mabweni ya Wanafunzi  na pia shule hiyo imebainika kuwa haina Matron kwa muda mrefu
Alisema  kwa sasa wanafunzi hao wanahifadhiwa kwa muda kwenye nyumba ya Matron hadi hapo bweni hilo litakapojengwa upya
Na ametoa agizo kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya na afisa elimu kuandika waraka kuziandikia shule zote 14 za bweni   kupinga matumizi ya mishumaa ,Taa na pasi za umeme kwenye mabweni
Mkuu huyo wa wilaya amefafanua kuwa jengo lililoungua lina thamani ya Tsh,Mil 40 na kuwa sasa wanaangalia ni kiasi gani cha fedha kinatakiwa kwa sasa kwa ajiri ya ukarabati na kuwa ni jukumu la Wananchi kuchangia ili bweni hilo liweze kurejea katika hari yake ya kawaida.
Mwisho